post

Wednesday, January 2, 2013

MSANII WA FILAMU ZA KIBONGO SAJUKI HATUNAYE TENA

Mwendazake Juma Kilowoka maarufu kama Sajuki enzi za uhai wake.
……………………………………………………

Mwigizaji wa Filamu Juma Kilowoka almaaruf kama Sajuki amepotezamaisha  alfajiri ya leo katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa baada ya hali yake kubadilika kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu, Sajuki alikuwa amelazwa katika wodi ya Mwaisela akipigania maisha yake katika hospitali hiyo.

Msanii huyo ameugua muda mrefu ambapo aliwahi kwenda India kutibiwa nchini India na baada ya kurejea kutoka mhuko afya yake iliimarika mpaka alipodondoka jukwaani tena katika tamasha la Bongo Movie jijini Arusha hivi karibuni.

Simon Mwakifwamba (kushoto) na wadau wengine wakimsaidia Sajuki (katikati) kutoka jukwaani baada ya kudondoka katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha mwishoni mwa mwaka jana.
Habari kutoka kwa  mmoja wa wanafamilia zimesema kwa sasa shughuli za kuhifadhi mwili wa mwendazake Sajuki katika hospitali ya taifa ya Muhimbili zainaendelea na ndugu kadhaa wamekusanyika nyumbani kwake Tabata .
Taarifa kamili zitakuijia mara zitakapopatinana kuhusiana na msiba na mazishi yatakapofanyikia.
Allan Kisoi Blog inawapa pole wanafamilia na wote waliofikwa na msiba huu.

No comments: