Sunday, April 29, 2012

MLIPUKO KANISANI WAUA 1 NA KUJERUHI 10

The scene at God House of Miracle Church in Nairobi, Ngara area where one worshipper died , ten others seriously injured in a grenade attack on April 29, 2012. PHOTO / William OeriMlipuko umetokea Jijini nchini kenya leo na kuuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine kumi.
Polisi wanasema guruneti lilirushwa kwenye kanisa la God's House of Miracle kwenye mtaa wa Ngara, wakati wa ibada ya asubuhi.Daktari mmoja katika Guru Nanak Hospital mjini Nairobi, ambako ndiko majeruhi walikopelekwa, aliwaelezea waandishi wa habari majeruhi aliowaona:

"Tumepokea majeruhi 7, mwanamke mmoja aliumia vibaya kwenye mguu wa kushoto, ambao umevunjika mahala kadha.

Mwanamme mmoja alikuwa na majaraha kadha kwenye nyama na tunafikiri amevunja mifupa piya; labda tukimfanyia x-ray tutatambua.

Kuna mama mmoja aliyevunja kidogo kisuguru cha mguu wa kushoto, na wengineo wamepata mikwaruzo-kwaruzo na kujikata-kata."

Kumetokea mashambulio kadha ya maguruneti nchini Kenya tangu mwaka jana pale serikali ilipotuma wanajeshi Somalia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu, Al-Shabaab.

No comments: